UTUNZAJI WA NGURUWE DUME – Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi


Utunzaji wa nguruwe mara nyingi hutegemea aina ya makundi ya nguruwe na mfunmo wa ufugaji. Makundi ya nguruwe ni kama madume ya mbegu, majike wazazi, watoto, na wale wanaonenepeshwa kwa ajili ya nyama au mafuta. Nguruwe wanaweza kufugwa ndani au nje ya banda, kutegemea na ukubwa wa shamba, kipato kilichopo kwa shughuli za ufugaji.

Ili kuleta mafanikio na tija katika ufugaji wa nguruwe ni vema kuzingatia utunzaji bora ikiwa ni pamoja na aina ya banda, uchaguzi wa nguruwe wazazi, ulishaji, udhibiti wa magonjwa na uangalizi kwa ujumla.

UTUNZAJI WA DUME LA MBEGU

utunzaji bora wa dume unaanza kwa kuchagua dume bora kwa ajili ya uzalishaji. Uchaguzi wa dume la kuzalisha ni muhimu kuliko uchaguzi wa jike kwa sababu dume moja hutumika kuzalisha nguruwe wengi katika kundi.

UCHAGUZI WA DUME BORA

Wakati wa kuchagua dume mfugaji anashauriwa kuzingatia yafuatayo:-
Achaguliwe kutoka kwenye koo wenye historia ya kukua haraka, kukuza watoto wengi na kuwatunza, kutokuwa na magonjwa au kilema cha kurithi.

  • Awe na miguu imara, mchangamfu na mwenye afya bora
  • Awe na umbile zuri linaloendana na aina yake na misuli imara itakayomwezesha kuoanda bila matatizo
  • Awe na kende mbili, kubwa, zilizokamilika na zinazolingana
  • Awe anayekua haraka na mwenye uwezo mkubwa wa kubadili chakula kwa matumizi ya mwili kuwa nyama
  • Awe na chuchu zisizopungua 12
  • Asiwe na mahisiano ya kinasaba (kama kaka na dada, mtoto na mama au mtoto na baba) na maike anayotegemea kuyapanda
  • Awe mrefu na mgongo ulionyooka

ULISHAJI WA DUME

Dume kwa ajili ya kupandisha apewe chakula bora chenye viini lishe vya kutosha vitakavyotosheleza mahitaji ya mwili bila kumfanya mnene sana au kukonda. Wakati wa msimu wa upandishaji alishwe chakula bora kiasi cha kilo 2.7 hadi 3.6 kwa siku.

PITIA
UFUGAJI WENYE TIJA: ANZA KUFUGA KUKU WATANO UPATE KUKU 200 NDANI YA MIEZI SITA

Wakati ambao sio msimu wa kupandisha, dume apewe chakula bora kiasi cha kilo 2 kwa siku. Kwa matumizi mazuri ya chakula hicho kigawanywe na kulishwa mara mbili kwa siku. Pia inatakiwa dume apewe maji safi na salama ya kutosha kila siku wakati wote.

KINGA DHIDI YA MAGONJWA NA WADUDU

Uzuiaji wa magonjwa na wadudu ni muhimu kwa afya ya nguruwe dume. Mfugaji anashauriwa kumwona mtaalam wa mifugo aliyekaribu nae ili kupata ushauri juu ya chanjo muhimu ka ajili kuzuia magonjwa kwa wanyama wake. Mfano kwenye sehemu ambazo ndorobo, mfugaji anashauriwa kutumia chanjo.

Kuzuia wadudu, mfugaji anashauriwa kuogesha nguruwe kwa dawa za kuogeshea angalau mara mbili kwa wiki ili kuzuia ukurutu na matatizo mengine ya ngozi. Kuzuia minyoo mfugaji anashauriwa kuwapa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu. Ni muhimu banda, vifaa vya kulishia na kunyweshea maji viwe safi wakati wote.

UTARATIBU WA KUTUMIA NGURUWE DUME KUPANDA

Upandishaji wa nguruwe unaweza kufanyika kwa njia mbili, ya kutumia dume au uhamilishaji. Njia ya kutumia dumendio inayotumiaka hapa nchni kwa utaratibu ufuatao:-

  • Nguruwe dume aruhusiwe kupanda kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miezi nane hadi kumi
  • Akiwa na umri wa miezi 10 hadi 18 anaruhusiwa kupanda mara moja kwa wiki
  • Akiwa na miezi 18 hadi 24 anaruhusiwa kupanda mara nne hadi tano kwa wiki
  • Dume wakubwa wasitumike kupanda majike wadogo kwani wanaweza kuleta madhara kama vile kuwavunja migongo.
  • Dume aruhusiwe kuendelea kupanda mpaka umri wa miaka 5 hadi 6

Mfugaji anashauriwa kuwa, ni muhimu dume la kupandisha liwekwe kwenye chumba chenye eneo la mita za eneo 9.3 ili kuweza kupata mazoezi ya mwili ikiwa sehemu ya kupanda imetenganishwa eneo liwe la mita mraba saba. Madume yatenganishwe na Majike ili kuepusha kupanda wakati usiotakiwa.

PITIA
DUME ZURI KWA UZALISHAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA

BANDA LA DUME

Liwe na ukubwa usiopungua 3 m * 2.5m geti liwe lachuma na linafunguka kuelekea kwa ndani na nje pande zote mbili, siku zote majike ya pelekwe kwa dume na si kinyume chake.

UPANDISHAJI

Madume huanza kupanda yakifikisha umri wa miezi 12 – 14 hupanda jike moja mara 2 kwa siku na hupanda majike 6 kwa kila siku 8 na majike yasifululize kwa zaidi ya siku mbili zinazofuatana, majike yapelekwe asubuhi mapema kabla ya dume kula chakula.

Dume linaweza kuendelea kutumika kwa upandishaji mpaka likifikisha miaka 3 – 4 ndipo unaweza kuanza kutumia dume lingine, uzoefu unaonyesha nguruwe chotara huwa na uwezo wa kupanda mara nyingi na kwa muda mrefu zaidi. Dume moja huweza kuhudumia majike 20 lakini kwa matokeo mazuri tumia dume moja kwa kila majike 15 – 18.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »