TAJIRIKA NA ZAO LA SOYA (GLYCINE MAX) – PART 1

http://mogriculture.blogspot.com/2016/06/tajirika-na-zao-la-soya-glycine-max.htmlSoya au Soybean (kwa kiingereza) ni zao la jamii ya mikunde. Kwa kitaalam linaitwa Glycine max. Zao hilo asili yake ni nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800 iliyopita. Zao la soya liliingizwa nchini Tanzania mwaka wa 1907 katika maeneo ya Amani mkoani Tanga.

1. HISTORIA, UMUHIMU NA AINA ZA SOYA

Historia ya zao la Soya nchini Tanzania

Soya au Soybean (kwa kiingereza) ni zao la jamii ya mikunde. Kwa kitaalam linaitwa Glycine max.

Zao hilo asili yake ni nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800 iliyopita. Zao la soya liliingizwa nchini Tanzania mwaka wa 1907 katika maeneo ya Amani mkoani Tanga. Kati ya miaka ya 1930 na 1960, kilimo cha soya kilipanuka na kuenea hadi maeneo ya Nachingwea mkoa wa Mtwara, Kilosa mkoa wa Morogoro na Peramiho mkoa wa Ruvuma. Kuenea kwa zao hilo katika maeneo hayo kulitokana na msukumo wa mashirika ya Overseas Food Co-operation – (OFC), State Trading Cooperation (STC), General Agricultural Production for Export – (GAPEX) naNational Milling Corporation – (NMC). Mashirika hayo yalisafi risha soya kwenda katika nchi za Japan na Singapore. Kwa kuwa uzalishaji wa zao hilo katika mikoa hiyo ulilenga soko la nje, wananchi hawakufundishwa matumizi yake na kwa sababu hiyo baada ya mashirika hayo kuacha biashara ya zao hilo kilimo cha soya kilifi fi a hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambapo uzalishaji ulianza tena baada ya jamii kuhamasika katika matumizi ya soya hasa katika kutengeneza vyakula vya watoto.

Umuhimu wa zao la Soya

Soya iliyokomaa

Soya ni zao lenye virutubisho vingi vya aina ya protini ikilinganishwa na virutubisho vya aina hiyo katika mazao mengine ya mimea na hata katika baadhi ya vyakula vinavyotokana na wanyama kama nyama na mayai na maziwa. Sifa hizo za soya zinafanya zao hilo, kuwa na umuhimu wa kipekee katika kutengeneza vyakula vya binadamu na mifugo na matumizi katika viwanda vya madawa na matumizi mengineyo. Mafuta yatokanayo na soya hayana lehemu (cholesterol) na hivyo kuwa na sifa ya kuboresha afya ya walaji.

Zifuatazo ni faida za kutumia soya:-

(i.) Soya ina virutubisho vingi na vilivyokamilika vya aina ya protini ambayo ni muhimu katika kuboresha lishe na afya kwa binadamu na mifugo;

(ii.) Soya ni chanzo rahisi na chenye gharama nafuu cha protini ambacho hata mtu wa kipato cha chini anaweza kumudu kwa kuwa zao hilo linaweza kulimwa maeneo mengi hapa nchini;

(iii). Kwa kuwa soya ina kiasi kikubwa cha protini ikilinganishwa na nyama na mayai na maziwa, inasaidia kupunguza kasi ya mashambulizi ya vijidudu vya maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kansa, moyo, na kuwaongezea nguvu wagonjwa hasa wa UKIMWI;

(iv.) Soya ni zao muhimu kwa watu wa kipato cha chini katika kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto kwa kuwa hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama na mayai;

PITIA
UFAHAMU UGONJWA WA KUKU WA KUVIMBA MACHO

(v.) Kutokana na uwingi wa protini, matumizi ya soya kwa watoto yanasaidia viungo kukua kwa haraka;

(vi.) Soya hurutubisha udongo kwa kutumia njia ya nitrogen fixation. Kwa hiyo ni zao linalofaa kutumika katika kilimo cha mzunguko (crop rotation) na katika kurutubisha ardhi ;

(vii.) Soya huongeza kipato na ni zao linaloweza kuchangia katika kuondoa umaskini kwa mkulima kutokana na gharama ndogo za uzalishaji. Aidha, ni zao linaloweza kuondoa umaskini kwa watengenezaji wa vyakula vya binadamu na mifugo, wafanyabiashara na wafugaji na kutoa ajira kwa rika zote yaani vijana na wazee, vijijini na mijini; na

(viii.) Utafi ti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa mafuta ya soya yanaweza kutumika kwa kuendeshea mitambo yaani bio-fuel na bio-diesel.

Aina za Soya

Kuna aina mbalimbali za soya, aina zilizozoeleka Tanzania na pamoja na:

Bossier, Uyole soya 1, Ezumu Tumu, Delma Hermon, Duiker na Kaleya.

Kila aina inahitaji mazingira na hali ya hewa inakowezakustawi, kukomaa kwa muda maalum na kutoa mavuno mazuri. Hata hivyo Bossier ni aina ambayo hustawi katika maeneo mengi nchini. Kwa wastani, aina mbalimbali za soya huchukua wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na aina, mahali ilikopandwa na utunzaji katika shamba.

  1. MAZINGIRA, MVUA NA RUTUBA YA UDONGO

Mazingira na mikoa inayofaa kilimo cha soya

Mmea wa soya uliozaa

Soya inaweza kulimwa katika sehemu zote zenye sifa na zinazofaa kwa kilimo cha maharage na mahindi. Sifa hizo ni pamoja na mvua ya kutosha, udongo usiotuamisha maji na udongo tifutifu usio na mchanga mwingi. Kutokana na kuwepo kwa maeneo mengi nchini yenye sifa hizo, ni dalili kuwa zao la soya linaweza kustawi katika maeneo hayo ambayo yapo karibu nchi nzima.

Jambo muhimu linalotakiwa ni kufahamu na kupanda aina za soya zinazofaa katika eneo husika kulingana na maelekezo ya wataalamu. Kwa sasa mikoa inayoongoza kwa kilimo cha soya ni Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa na Morogoro. Mikoa mingine yenye uwezo na sifa za kuzalisha soya ni Tanga, Mtwara, Lindi, Kagera, Mara, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na Wizara ya Kilimo na Chakula mwaka wa 2005, zaidi ya tani milioni mbili za soya zinaweza kuzalishwa kwa mwaka endapo maeneo yote ya nchi yanayofaa kwa kilimo cha soya yakitumika ipasavyo. Uzalishaji wa sasa unakadiriwa kuwa tani elfu tano (5,000). Kiwango hiki cha uzalishaji ni cha chini sana ukilinganisha na kiwango kinachoweza kufi kiwa. Aidha, kiasi hiki kidogo na uwezo unaoweza kufi kiwa ni changamoto katika kuongeza uzalishaji na matumizi ya zao hilo.

Mahitaji ya Mvua

Soya huhitaji wastani wa mililita 350 hadi 1,500 za mvua kwa mwaka na inayonyesha kwa mtawanyiko mzuri hususan katika kipindi chote cha ukuaji wa zao hilo. Soya pia inafaa katika kilimo cha umwagiliaji kwani katika maeneo hayo kunakuwa na uhakika wa unyevu muda wote. Jambo la kuzingatia ni kutowepo kwa mvua wakati soya inapokauka.

PITIA
KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO

Rutuba ya Udongo na Mahitaji ya Mbolea

Mmea wa soya kabla haujazaa

Kama ilivyo kwa mazao mengi, soya pia huhitaji udongo wenye rutuba na usiotuamisha maji. Hivyo endapo soya italimwa katika sehemu yenye rutuba hafi fu, itahitaji mbolea kama mazao mengine ijapokuwa huvumilia udongo wenye rutuba hafi fu. Kwa hiyo uamuzi wa kutumia au kutotumia mbolea na kiwango cha kutumia utategemea rutuba iliyopo kwenye udongo katika eneo husika. Hata hivyo, soya huhitaji wastani wa kilo 80 hadi 100 za mbolea aina ya DAP na TSP kwa hekta moja na kilo 60 hadi 80 kwa mbolea aina ya CAN kwa hekta moja. Mtaalamu aliyepo karibu na mkulima anaweza kushauri hali ya rutuba ya udongo katika eneo husika. Jambo la kuzingatia wakati wa kupanda ni kuhakikisha kuwa mbolea haigusani na mbegu kwa sababu mbolea itaunguza mbegu na hazitaota. Samadi iliyoiva pamoja na mbolea nyingine za asili pia zinafaa kutumika katika kilimo cha soya.

  1. UTAYARISHAJI NA UTUNZAJI WA SHAMBA LA SOYA

Kutayarisha shamba

Shamba la soya linahitaji maandalizi mazuri kama ilivyo kwa mazao mengine. Utayarishaji huo wa shamba ni pamoja na kuondoa magugu yote kwa kuwa soya haivumilii magugu hasa ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji (seedling stage).

 

Shamba la soya linaweza kulimwa kwa sesa au matuta. Kilimo cha sesa chaweza kulimwa kwa kutumia jembe la mkono au la kukokotwa na wanyama kazi kama maksai na punda au kwa kutumia trekta. Kilimo cha matuta kukinga mteremko kinafaa na kinapendekezwa kwa maeneo yenye mwinukoVilevile kilimo cha matuta kinafaa sehemu tambarale lakini zenye mvua nyingi ili kupunguza madhara ya maji yanayotuama baada ya mvua kubwa kunyesha.

Mbegu

Ni muhimu kuandaa mbegu bora na safi mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza. Kwa wastani kilo 20 hadi 30 za mbegu za soya zinatosha kwa hekta moja kutegemeana na aina ya mbegu. Kwa kuwa aina nyingi za soya hazistawi kila mahali, ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha kuwa anatumia mbegu inayofaa katika eneo analotaka kulima soya hususani mahitaji ya mvua. Kwa sababu hiyo ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri toka kwa mtaalam aliyekaribu naye kabla ya kuamua kulima soya. Aidha, mkulima anashauriwa kununua na kutumia mbegu kutoka katika sehemu ambazo chanzo cha mbegu hizo kinaeleweka. Mfano wa sehemu hizo ni pamoja na maduka ya pembejeo, wakala wa mbegu, mashamba ya mbegu na vituo vya utafi ti. Hii ni kwa sababu mbegu ya soya hupoteza nguvu ya uotaji katika msimu mmoja hasa katika sehemu za joto. Kwa hiyo mkulima anatakiwa kuhakikisha kuwa anapanda mbegu itakayoota. Kama mkulima hana uhakika na chanzo cha mbegu au ana wasiwasi wa kuota kwa mbegu alizonazo anaweza kufanya majaribo ya uotaji (germination test) kabla ya kupanda. Njia rahisi ni kuzilowesha mbegu kwa maji na kisha kuziweka kwenye kitambaa mahali penye joto la kutosha. Mbegu ziloweshwe na maji kila siku mpaka zitakapoota. Hesabu mbegu zilizoota na iwapo mbegu zilizoota ni chini ya 75 kati ya mbegu 100 yaani asilimia 75, mkulima anashauriwa kutopanda mbegu hizo.

PITIA
UCHANGANYAJI WA VYAKULA VYA MIFUGO

Wakati wa kupanda

Upandaji wa soya unategemea na aina na mahali husika. Kwa aina za soya zinazokomaa mapema, soya ikipandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua katika maeneo yanayopata mvua kwa kipindi kirefu itakomaa wakati mvua bado zinaendelea kunyesha na hivyo kufanya uvunaji na ukaushaji kuwa mgumu na kuhitaji nguvu kazi na muda wa ziada la sivyo mbegu zitaoza au kuanza kuota na kupoteza ubora wake. Kwa hiyo ni budi kujua mwenendo wa mvua mahali husika ili kupanda kwa wakati na aina ya soya kulingana na mahali hapo. Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa soya inakomaa wakati hakuna mvua ili kurahisisha uvunaji na soya kutooza. Jedwali Namba 1 linaonyesha mahali, aina na muda wa kupanda soya.

Jedwali Namba 1: Muda unaoshauriwa kupanda soya

 

Na. Mahali Mbegu Muda
1 Sumbawanga, Nkasi, Songea,
Mbeya, Njombe, Dabaga na sehemu Uyole soya 1 Novemba/Desemba
zenye mvua nyingi/ndefu
2 Sumbawanga, Songea, Mbeya,
Njombe na sehemu zenye mvua     Bossier Januari
nyingi/ndefu
3 Ileje, Mbarali, Chunya, Mtwara na
sehemu zenye mvua kidogo na fupi     Bossier Novemba/Desemba
4 Morogoro na Tanga Bossier Februari na Machi

Nafasi ya kupanda

Mmea wa soya baada ya kuota

Mkulima anashuriwa kupanda soya kwa nafasi zinazo pendekezwa na wataalamu. Nafasi hizo ni sentimeta 10 kwa sentimita 45 kwa soya fupi kama bossier na kwenye sehemu zenye rutuba hafi fu. Aidha, tumia sentimeta 10 kwa sentimita 60 kwa soya ndefu kamaUyole Soya 1 na kwenye sehemu zenye rutuba nyingi.

Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa kina cha sentimeta mbili hadi sentimita tano ili zisiharibiwe au kuliwa na wanyama kama panya. Mkulima ahakikishe kuwa soya inapandwa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha; haitakiwi kabisa kupanda soya kwenye udongo mkavu au kuloweka soya kabla ya kupanda.


Palizi

Soya ni zao ambalo huzongwa na magugu hususani ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi palizi katika kipindi cha wiki mbili baada ya soya kuota. Palizi ya mara ya pili inategemeana na kiwango cha magugu shambani. Endapo magugu yatakuwa yamefunikwa na majani ya soya palizi ya pili inaweza isihitajike kwa kuwa soya iliyopandwa kwa nafasi zinazotakiwa hukua na kufunika magugu yote na hivyo palizi ya pili kutohitajika.

Soya ikipandwa kwa nafasi pana na isiyotakiwa haikui kufi kia kiwango cha kufunika magugu na hivyo kulazimisha palizi ya pili kufanyika. Magugu katika shamba la soya yanaweza kudhibitiwa pia kwa katumia dawa ya kuzuia magugu kama GALEX; hata hivyo inafaa kufuata maelekezo ya kutumia ya dawa husika.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO BORA CHA ULEZI

Ulezi ni punje ya mlezi au mwele (aina ya nafaka) ambao hulimwa katika sehemu zenye hali ya ukame. Ulezi ni zao la asili, shirika la

Read More »

Kilimo Bora Cha Alizeti

Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »