JINSI YA KULEA VIFARANGA VYA KUKU SEHEMU YA KWANZA(1)

Karibu mpenzi msomaji wa KILIMO TANZANIA , leo hii napenda kuwaletea soma la jinsi ya kulea vifaranga vya kuku, hivyo tusiache kua nasi ili kujifunza mengi zaidi.
Na tutaanza na jinsi ya kujenga nyumba ya vifaranga, hivyo ukitaka kujenga nyumba ya vifaranga nilazima uzingatie yafuatayo.
  • Nyumba ya vifaranga nilazima ijengwe karibu na nyumba ya muangalizi hii ni kwaajiri ya kuweza kuwa karibu kwa uangalizi zaidi.
  • Nyumba ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa hii nikwaajili ya kupunguza maambukizi ya magonjwa.
  • Nyumba ya vifaranga isiruhusu unyevu, baridi na wanyama au wadudu kuingia ndani, lakini ni lazima iwe na mwanga wakutosha
  • Pia nyumba ya vifaranga inatakiwa kua na uwazi wa kutosha kuwezesha vifaranga kutobanana na waweze kutembea kwa uhuru.
  • pia ijengwe eneo ambalo haliruhusu upepo kutoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa kuingia hii itapunguza maambukizi ya magonjwa.
 UKUBWA WA NYUMBA
Ukubwa, vifaranga hawaitaji eneo kubwa katika wiki 4 za mwanzo, kwa makidirio mazuri mita squire moja huchukua vifaranga 16, na baada ya wiki 4 za mwanzo unatakiwa kuongeza eneo ili kuwapa nafasi zaidi.
Sakafu, sakafu inayo faa ni ile ya simenti ikichanganywa na zege au unaweza kuchukua kinyesi cha ng’ombe kilicho changanywa na maji kisha ukasiliba chini, unaweza kuchagua aina gani ya sakafu kati ya hizo kulingana na uwezo wako.
Ukuta, unaweza kujenga ukuta kwa kutumia matofari, bati, mabanzi au debe kulingana na uwezo wako, urefu unatakiwa kua futi 6-8 kutoka chini kwenda juu futi 3-4 za chini nilazima zizibwe na ukuta na futi 3-4 za juu unaweka wavu wa chuma au fito kulingana na uwezo wako, na ukuta ulio jengwa kwa tofari nilazima upigwe lipu.
Dirisha, madirisha yanaweza kuzibwa kwa kutumia mabokis au mkeka ikishwa wekwa nyavu, kulingana na uwezo wako.
Paa, Paa nilazima liwe zuri lisilo vuja na unaweza kuweka tundu la kutoa hewa y joto
Nitumaini langu umepata elimu ya kutosha na usisite kua nasi ili kuendelea kupata elimu zaidi.
PITIA
MATUMIZI YA UHAKIKA YA DAWA ZA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI WA MIFUGO

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo bora cha Ndizi

Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa

Read More »

CORONA VIRUS EDUCATIONAL POST

Naomba twende polepole Vyanzo vya vifo duniani na idadi (WHO, 2019) Heart diseases – mil 9.43Stroke – mil 5.73COPD – mil 3.04Pumu – mil 2.96Alzheimer’s

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »