Hizi ndizo Faida ya kutumia mbolea katika kilimo cha maharage

Kuna faida kubwa sana pale unapotumia Mbolea katika kilimo cha zao lolote, Watu wengi wamekuwa wakipuuza kutumia mbolea katika kilimo cha maharage huku baadhi yao wakiwa hatambua kama ipo haja ya kutumia mbolea katika kilimo hicho, ila ukweli ni katika mazao ni kwamba maharage hayahitaji nitrogen kwa wingi kwa sababu mizizi ya maharage husaidiana na viumbe hai (nitrogen fixing bacteria) waishio kwenye udongo kutengeneza nitrogen.

Hata hivyo maharage yanahitaji phosphorus ambayo hupatitikana katika mbolea kwa ajili ya kuboresha mizizi na potassium kwa ajili ya kuuandaa mmea kwa ajili ya kutoa maua mengi na kuzaa matunda bora.

Ikiwa shamba lililimwa zao ambalo liliwekwa mbolea kama vile Urea au CAN basi huna haja ya kuweka tena mbolea za nitrogen badala yake unaweza kuweka TSP au DAP Kg 60 kwa hekta wakati wa kupanda. Au mbolea ya minjingu (Minjingu Rock Phosphate) Kg 250 kwa hekta moja wakati wa kupanda.

Kama shamba limechoka sana au halikuwekwa mbolea za nitrogen msimu uliopita basi tumia NPK katika uwiano wa 5:10:10 kiasi cha Kg 30 kwa hekta, nayo iwekwe wakati wa kupanda. Mbolea zote ziwekwe sentimita tano hadi 10 kutoka kwenye shina/shimo la mmea na urefu wa sentimita 3 hadi 5 kwenda chini.

Pia unaweza kutumia mbolea ya zizi/samadi (tani 5 – 10 kwa hekta) au mbolea ya kijani (green manure, tani 5 kwa hekta). Mwaga/tawanya samadi kwenye shamba lote halafu ichangane vizuri na udongo kwa kulima kwa plau (la tractor au ng’ombe). Maana yake ni kwamba mwaga samadi kabla ya kulima shamba lako kwa trekta/ng’ombe.

Mbolea ya kijani inapatikana kwa kusafisha shamba halafu ukaliacha mpaka majani/magugu yakaota kisha ukalilima kwa trekta au ng’ombe (likiwa na magugu hivyo hivyo) lakini kabla hayajatoa mbegu halafu ukapanda. Mbolea ya minjingu inaweza kutumika pamoja na samadi na mbolea ya kijani.

PITIA
KANUNI NA ULIMAJI WA KILIMO BORA CHA ZAO LA MAHINDI.

Lakini lincha ya kueleza ya kwamba maharage yanahitaji mbolea kwa wingi kama ambavyo nimeeleza hapo awali,

Maharage huhitaji mvua ya kutosha kipindi cha kabla ya uwekaji maua (before flowering) na kipindi cha ukuaji wa vitumba vya maharage (podding). Huhitaji unyevu kidogo kipindi cha kuweka maua (during flowering) na ukavu kipindi cha kukomaa (pod maturation) na kukauka vitumba.
Vitumba ni matunda (pods). Ikiwa utatumia njia nyingine yoyote ya umwagiliaji angalia maharage yako yapo katika hatua gani kabla hujapanga ratiba yako ya umwagiliaji (irrigation schedule

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

ZIJUE FAIDA ZA KULIMA MAPAPAI

Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica papayaPapai ni moja ya matunda ambayo huchukua

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »